Radio Taifa: Daluga ya spoti – Kothbiro yaingia awamu ya 16

Michael Olunga. Picha/Goal

Makala ya 47 ya mashindano ya kila mwaka ya KothBiro kwa timu za kutoka mitaa ya Nairobi yataingia hatua ya awamu ya 16 bora Disemba 27.

Aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Raga Charles Cardovillis ambaye kwa sasa anajiuhusisha na usimamizi wa wa maswala ya michezo, amesema wanaangazia kuhakikisha yanaandaliwa kote nchini katika kaunti 47 kuanzia mwaka ujao kabla ya kumalizia kwa fainali ya kitaifa baada ya kupigwa jeki kutoka kwa kampuni ya Betmoto.

Mashindano hayo yamewakuza nyota wengi wa soka humu nchini kama vile Victor Wanyama, Dennis Oliech, Dan Shikanda, Mahmoud Abbas, Michael Olunga na Jamal Mohammed miongoni mwa wengine.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *