Radio Taifa: Vijana zaidi ya elfu 280 waajiriwa kazi mtaani

Zaidi ya vijana elfu 280 kote nchini wamenufaika na mradi kazi mtaani katika awamu ya pili iliyozinduliwa mapema wiki hii.

Mradi huo wa kutoa huduma za usafi katika mitaa ya mabanda nchini, umeenezwa katika kaunti zote 47 katika awamu ya pili.

Kwenye bajeti ya kifedha ya mwaka 2020/2021,serikali ilitenga shilingi bilioni 10 kwa mradi huo ambao unawaajiri vijana ,walemavu na watu wenye mahitaji maalum wanaolipwa mshahara kila siku .

Kulingana na Patrick Bucha ambaye ni katibu katika idara ya nyumba inayosimamia mradi huo,awamu ya pili inatazamiwa kukamila katika kipindi cha miezi sita na unaendeshwa kwa ushiriakiano wa serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zote 47.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *