Watu 38000 wananufaika na mpango wa malipo ya moja kwa moja kutoka kwa serikali

watu 38000 wananufaika na mpango wa malipo ya moja kwa moja kutoka kwa serikali, yani cash transfer,kutoka kwa serikali kuu, huku wanaolengwa hasa wasiojiweza, waliolemaa na wakongwe wakipata shilimgi elfu moja kila wiki.  huku vijana 16,758 kutoka kaunti ya Mombasa wakinufaika na mpango wa kazi mtaani.

Akizungumza na Dalila Athman katika kipindi Uchambuzi na swala nyeti, kamishna kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo, ameeleza kuwa mpango huo wa serikali ulianzishwa ili kusaidia kupunguza makali ya athari ya homa ya Corona, kila kijana anapata shilingi 455 kila siku baada ya kuanza kwa awamu ya pili ya mpangu huo. Amesema kamati maalum inayojumuisha machifu na wazee wa mitaa ndio inayosimamia kuandikishwa kwa walengwa,


Kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya Corona katika kaunti ya Mombasa,  Kitiyo amedokeza kuwa idadi ya maabukizi imeshuka lakini ametahadharisha wakaazi dhidi ya kupuuza maagizo ya serikali ya kujikinga na virusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *