Wagombea wote wa eneo bunge la Msambweni wachunguzwe

Baadhi wagombea wa kiti cha ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni wanaunga mkono wito wa kuchunguzwa kwa wagombea wote kimaadili kabla kuruhusiwa kuingia debeni.
Akiongea na pwani Fm Charles Bilali aliyemiongoni mwa wagombea waliojitokeza anasema viongozi ambao hawana maadili wamekuwa wakitumia njia za mkato kujipata uongozini, jambo ambalo amelitaja huchangia kuzorota kwa maendeleo hasa eneo hilo.
Bilali amesema anaamini endapo tume ya maadili na kupambana na ufisadi itafanya kazi yake sawa sawa kuwachuja wagombea hao kwa misingi ya kimaadili ni wachache watakao ruhusiwa kuingia debeni.
Aidha Bilali amewataka wananchi wasikubali kutumika kisiasa kuwazushia lawama baadhi ya wanasiasa kwa misingi ya kisiasa, akisema kila atakaye toa kashfa za uongo awe tayari kusimama mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya madai watakayo-toa.
Uchaguzi huu mdogo wa eneo bunge la Msambweni tayari umewavutia wagomeaji wengi, wanacho jiuliza wakenya ni kwamba je, tume ya maadhili na kupambana na ufisadili itauoikea wito huu?
Na kama itaupokea je, unaona kunauwezekano wa baadhi ya waliojitokeza kufungiwa nje ya kinyang’iro hiki kutokana na historia zao za kimaadili?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *