Shirika la WHO linafanya kazi kwa karibu na kamati ya kitaifa ya dharura ya kupambana na corona

Mtaalamu anayejishughulisha na magonjwa ya kuambukiza wa shirika la Afya duniani(WHO), Dkt Joyce Onsongo amesema shirika hilo linafanya kazi kwa karibu na kamati ya kitaifa ya dharura ya kupambana na corona kwa kutoa mchango wa vifaa vya kupima sambamba na ufuatiliaji wa sera za kudhibiti virusi hivyo.
Dkt Onsongo pia ameelezea mikakati wa WHO katika kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona humu nchini.
Kuhusu ugonjwa wa corona kutoa dalili nyingine kuliko zile zinazofahamika,Dkt Onsongo ameweka wazi kuwa upo utafiti kufuatilia dalili hizo huku akieleza matumaini ya kupatikana kwa chanjo.

One Reply to “Shirika la WHO linafanya kazi kwa karibu na kamati ya kitaifa ya dharura ya kupambana na corona”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *