Uhasama baina ya Harmonize na lebo yake ya zamani WCB unazidi

Kwa kweli maneno mtaani ya chu chu chu Ila leo kitendo ndio ujumbe wa meneja wa msanii Diamond Platinumz Sallam SK wakati alipokataa waziwazi kupokea mkono wa salamu kutoka kwa aliyekua msanii wa WCB Harmonize katika hafla ya mazishi ya mkewe Babu Tale, Shamsa Kombo mjini Morogoro hii leo.
Harmonize aliwasili katika mazishi nakupatana na waombolezaji waliokua wamekaa.
Katika moja ya chandarua ya VIP mmoja wao alikua Sallam SK.
Baada ya kuwasalimia baadhi ya wageni hatimaye msanii huyo alikutana ana kwa ana na meneja wake wa zamani.
Ni muda tangu wawili hao wakutane katika sehemu kama hizo na wengi walitegemea matukio sawia na hayo.
Lakini ilipofika wakati wakusalimiwa Sallam aliupiga mkono wa Harmonize ishara tosha kuwa uhasama baina ya Harmonize na lebo yake ya zamani WCB unazidi kutokota.
Wanasema matendo yanazungumza kuliko maneno

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *