Mjane anayefua nguo ili kulea watoto wake

Ulimwengu umeadhimisha siku ya wajane hii leo. Umoja wa mataifa unakadiria kuwa kuna wanawake zaidi ya milioni 115 duniani wanaoishi kwenye lindi la umaskini huku wengi wakipitia changamoto za kitamaduni kama kurithiwa na mali zao kurithiwa na jamaa zao na kuwachwa bila namna Mariam Mutiso kutoka mtaa wa Chaani kaunti ya Mombasa ni miongoni mwa wanawake hawa.

Mwanahabari Sylivester Chibero alizungumza naye na  anatusimulia jinsi anavyojikimu kimaisha baada ya mumewe kufariki. Mama huyu anafanya kibarua cha kufua nguo. Amekifanya kwa miaka mingi sana ili kulea watoto wake


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *