Vanessa Mdee “nilikuwa mlevi sana”


Kupitia Podcast hiyo Vanessa Mdee ameeleza mambo mengi sana aliyopitia kwenye muziki wa bongo Fleva hadi kufikia hapa alipo kwa sasa, Kupitia Audio hiyo aliongezea kuwa muziki wa Bongo Fleva ni demonic akimaanisha muziki ni Pepo.Mbali ya kuzungumzia kuachana na muziki Vanessa pia ameeleza alivyopitia wakati mgumu hadi kujiingiza kwenye ulevi wa pombe kisa muziki lakini pia alipishana kauli na mama yake baada ya kujiingiza kwenye muziki, akiongeza kuwa mama yake ni mtu wa dini hivyo aliamini mwanae kama anapotea hivi kutokana na kile alichokuwa akifanya Vanessa.
Vanessa pia aliongezea kuwa anafahamu atawakwaza watu wachache ila ni sawa tu, anajua mashabiki zake hawataki kusikia hili lakini wavute picha, hayupo mbali sana na wao, Sababu za kwanini ameamua kuachana na muziki ni kwa sababu alihitaji kuchagua maisha yake, huu muziki ni pepo (demonic) “Najua wengi watajiuliza kuhusu hiki kwamba hivi Vnessa hataimba tena, au hatutakuona tena ukitumbuiza na kufanya muziki, Kiukweli mimi Napenda muziki, napenda kutumbuiza, hiki ndicho kitu ambacho nimeletwa kukifanya duniani, Ukweli ni kwamba labda nililetwa kupitia hii tasnia ili nije nikusimulie kwa uaminifu, ukweli kuhusu vitu ambavyo huwezi kuambiwa sehemu yoyote”
Mambo mengi sana amesimualia Vanessa mdee hasa yale yanayosikitisha kuhusu tasnia ya muziki aukweli wake lakini pia hali ngumu aliyopitia kwenye maisha ya muziki, Lakini Vanessa alimaliza kwa kusema kuwa kwa sasa anaishi nchini Marekani na mpenzi wake Rotimi katika mjengo ambao mpenzi wake huyo ameununua huko Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *