Nancy Karigithu aweka wazi mikakati inayotumika katika ubahariaKatibu katika Idara ya Usafirishaji na  Maswala ya baharini, katika wizara ya uchukuzi na miundo msingi Nancy Karigithu amesema mikakati kabambe imewekwa ili kuona kwamba shughuli za ubaharia kwenye meli hazisitishwi.
Akizungumza na Pwani Fm kwa njia ya simu Karigithu amesema kwamba lugha ya kingereza ni mojawapo ya masharti yanayo hitajika katika kazi ya ubaharia, kwani lugha hiyo inatumika wakati wanapotafuta ajira katika sekta hiyo.
Hata hivyo walio kwenye meli wataendelea kusalia huko ili kuzuia kutengamana na watu hali ambayo inaweza kuchangia maambukizi zaidi

Aidha Karigithu amesema meli zitaendelea kufanya kazi licha ya ulimwengu kushuhudia msambao wa virusi vya korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *