Pwani Mchana : Waziri wa fedha Ukur Yattani ametengea serikali za kaunti shilingi bilioni 369.9
Waziri wa fedha Ukur Yattani ametengea serikali za kaunti shilingi bilioni 369.9 katika kipindi cha matumizi ya pesa za serikali cha mwaka 2020/2021.

Serikali inabuni mpango wa kiuchumi wa baada ya janga la virusi vya Corona ili kukabiliana na athari mbaya za kiuchumi za janga hilo na kurejesha uchumi kwa mkondo wa kufufuka.

Baadhi ya wanachama wa muungano wa ANC kutoka kaunti ya Mombasa wamemkashifu katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna kwa madai ya kumkejeli kiongozi wao Musalia Mudavadi kwa misingi ya kumzuia azma yake ya kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *