Budget ya kenya kugharimu trillion 3.2

Waziri wa fedha, Ukur Yatani leo lasiri atawasilisha bajeti ya kitaifa ya shilingi trilioni-3.2 katika kipindi cha mwaka 2020/2021 ambacho kitaanza tarehe moja Julai.

Siku ya Jumanne, kamati ya bunge kuhusu bajeti iliidhinisha matumizi ya shilingi trilioni-1.80 ambapo shilingi bilioni-584.9 zitafadhili miradi ya maendeleo na shilingi bilioni-316.5 zitatolewa kwa serikali za kaunti.

Na katika eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale mseto wa hisia pia unazidi kutolewa kuhusu mgao wa bajeti ya shilingi trillioni 2.7.

Wakaazi hao wamependekeza kwamba sekta za kilimo na utalii zipewe mgao wa kutosha katika makadirio ya bajeti hiyo ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021 ili waweze kumudu bei ya vyakula na ajira kwa wakaazi wanaotegemea sekta ya utalii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *