Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki kutokana na matatizo ya moyo akiwa na umri wa miaka 55.
Serikali ya taifa hilo yasema kuwa alifariki akipata matibabu katika hospital moja nchini humo alipolazwa siku ya Jumamosi na kisha kukabiliwa na matatizo ya moyo na kufariki siku ya Jumatatu
Rais huyo alikuwa astaafu Mwezi Agosti. Ameongoza taifa hilo kwa miaka 15.
Mkewe Denise Nkurunziza yuko hapa nchini ambapo anapata matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi anatibiwa maradhi ya Covid 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *