Pwani Mchana : Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi aeleza mabadiliko ya chama cha ODM

Chama cha walimu wa shule za upili KUPPET kimetoa wito kwa wizara ya elimu itenge sehemu ya shillingi milioni 700 za hazina ya shughuli za michezo ya shule ili ziweze kulipa mishahara ya walimu walioajiriwa na bodi za wasimamizi wa shule.
Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ameeleza kuwa mabadiliko yanayoendelea ndani ya chama cha ODM ni kawaida na kwamba ni njia mojawapo ya kukisafisha chama sawa na kuweka mipangilio mwafaka chamani.